- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na Shani Amanzi,
Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa wa Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus Mashimba amepokea msaada kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa Mkoa wa Dodoma Bi.Rehema Madenge kwa ajili ya walioathirika wa Mafuriko yaliyotokea Januari, 2018 katika kijiji cha Olboloti na Mrijo chini kata ya Mrijo Wilayani Chemba.
Bi.Rehema Madenge amekabidhi msaada huo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kamati ya Maafa, ambapo aliwapa pole wote waliopata maafa hayo na kusisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ipo pamoja nao kuwapa pole na kutoa misaada mbalimbali kwani janga hili ni la Taifa.
Bi.Rehema aliongeza kwa kusema “kinachotakiwa ni Wananchi mchukue hatua za haraka kuhama eneo la bondeni ili kuepuka athari zingine kwa sababu bado mvua zinaendelea kunyesha na Mwenyekiti wa kamati ya Maafa wa Wilaya hakikisha zoezi hili linafanyika haraka ili Wananchi hawa waliothirika wapatiwe viwanja na maisha yao yaendelee kama kawaida.”
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa wa Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus Mashimba ameishukuru Serikali kwa kutoa msaada huo na kuahidi kuendelea kuwa bega kwa bega na Wananchi wake katika kutoa huduma za kimaendeleo ikiwemo kuwapatia viwanja wananchi wote waliopata Maafa ya Mafuriko katika kata ya Mrijo chini.
Kamati ya Maafa ya Mkoa wa Dodoma na Kamati ya Maaafa ya Wilaya ya Chemba wametembelea kata ya Mrijo tarehe 26/1/2018 katika kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vikiwemo mablanketi, ndoo, mikeka na mahema kwa waliothirika wa mafuriko ya mvua iliyonyesha Januari, 2018.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.