- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na ShaniAmanzi,
Mkuu wa Wilaya wa Chemba Mhe.Simon Odunga amewataka Watendaji na Wataalam wa Halmashauri kusimamia Sheria ndogo za angazi za kata na vijiji katika kuendelea kusimamia na kuthibiti uharibifu wamazingira.
Mhe.Saimon Odunga amesema “ikiwa leo ni siku ya Mazingira Duniani na utaratibu huu hufanyika kila mwaka kuanzia tarehe Juni mosi hadi juni 05 hufanyika maadhimisho haya,kwa hiyo ni lazima kuzuia viashiria hivyo ikiwemo ukataji wa miti ovyo kwa ajili ya uchomaji mkaa na kuni,uchomaji moto ovyo misitu,utupajiti taka ovyo,kilimo katika maeneo ya miteremko mikali na uchimbaji wa mawe”
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chemba Dkt.Semistatus Mashimba amesema Halmashauri ya Chemba kwa kushirikiana na Wakalawa Misitu Tanzania (TFS) wanaendelea na Kampeni ya kupanda miti ndani ya Wilaya ya Chemba.
“Kwa mwaka huu wa 2018-2019 tunatarajia kupanda miti laki tano ,hii ni utekelezaji wa mpango ulio asisiwa na Makam wa Rais,Mh. Samiah Suluhu wa kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa wa kijani sambamba na kuisaidia jamii kupata nishati ya kupikia kama vile kuni”aliongeza kwa kusema hivyo Dkt.Mashimba.
Kwa upande wa Mkuu wa Idara ya Usafina na Mazingira wa Halmashauri ya Chemba Ndg.Mohamed Semdoe amesema kwa kushirikiana naViongozi katika ngazi za Kata naVijiji ,tunaendelea kushiriki katika zoezi la usafi wa mazingira kila siku ya Jumamosi ya mwisho wa mwezi.
Pia Idara ya Usafi na Mazingira imeanzisha mkakati wa kutenga maeneo ya dampo katika ngazi za vijiji pamoja na kuhamasisha jamii zishiriki katika kuchangia gharama za uzoaji taka kutoka katika maeneo ya makazi na biashara.
Kauli mbiu ya mwaka huu Kitaifa ni “MKAA NI GHARAMA;TUMIA NISHATI MBADALA”.Maadhimisho ya wiki ya siku ya Mazingira duniani yamefanyika 05/06/2018 katika kijiji cha Kidoka Wilayani Chemba.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.