- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe. Halima Okash amewataka Watendaji wa Vijiji na Kata kuitisha mkutano na kuwasomea Wananchi mapato na matumizi pamoja na kuwafahamisha kuhusu fedha zilizopokelewa na miradi itakayotekelezwa kutokana na fedha hizo.
DC Okash ameyasema hayo Julai 15, 2025 akiwa katika ziara ya kusikiliza na kutatua kero za Wananchi Kata ya Makorongo na Kata ya Gwandi Wilayani Chemba.
"Wananchi wana haki ya kujua fedha zinazopokelewa, miradi iliokusudiwa na kufuatilia ubora wa miradi hiyo kama inaakisi gharama halisi " Amesema DC Okash.
Aidha Mhe. Okash amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imewekeza fedha nyingi katika sekta ya elimu ili kuwawezesha Watoto wote kupata elimu bure kuanzia ngazi ya msingi, na sekondari ambapo pia Serikali inatoa mikopo kwa elimu ya juu, hivyo amewataka Wazazi na Walezi kuzitafuta fursa za elimu kwa Watoto kwakuwa urithi mzuri wa Mtoto ni elimu ili aweze kujisimamia na kuwasaidia Wazazi kusimamia shughuli za maendeleo.
"Chemba itajengwa na Wanachemba wenyewe, Chemba haitajengwa na Wageni somesheni Watoto wenu waje kuwasaidia kusimamia maendeleo katika Wilaya yenu" Amesema Mhe. Okash.
Sambamba na hilo, Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa Serikali ngazi ya Wilaya inatarajia kufanya sensa ya mifugo na utambuzi wa Wakulima ambapo pia amewataka Wafugaji kufuga kisasa na Wakulima kulima kisasa na kuachana na ufufugaji na kilimo cha mazoea
Hata hivyo, Mtendaji wa Kata ya Makorongo Ndugu Andrew Chilewa amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hssan kwa kuwezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali katika Kata hiyo ikiwa ni pamoja na miradi ya Afya, miradi ya elimu, Maji, barabara na kupeleka Watumishi 12 ambao wanaendelea kuwatumikia Wananchi.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.