- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
DC CHEMBA ASIKILIZA NA KUJIBU KERO ZA WANANCHI KATA YA CHANDAMA NA SONGOLO.
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe. Halima Okash Julai 10, 2025 amefanya ziara ya kusikiliza na kujibu kero za Wananchi wa Kata ya Chandama na Kata ya Songolo Wilayani Chemba.
Mara baada ya kujibu kero za Wakazi wa Kata hizo DC Halma Okash amewataka Wakazi wa Kata hizo kubadili mtazamo wao kuhusu elimu,waone umuhimu wa elimu kwa Watoto wao ili kuwatengenezea mazingira mazuri ya kujitegemea na kuongeza kuwa hakuna urithi mzuri kwa Watoto zaidi ya elimu.
Sambamba na hilo DC Okash amewasisitiza Wazazi kuhusu umuhimu wa kuchangia chakula cha Watoto wao Shuleni ili kuongeza kiwango cha uelewa na ufaulu kwani ni vigumu sana kwa Watoto kusoma na kuelewa vizuri masomo yao wakiwa na njaa.
DC Okash pia amewaomba Wazazi kuwapa ushirikiano Walimu ili waweze kuwasomesha vizuri Watoto badala ya kuwavunja moyo Walimu hao.
Kuhusu utunzaji na ufuatiliji wa miradi ya maendeleo Mhe. Okash amesema kuwa Wananchi wanao wajibu wa kutunza na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao kwani Serikali inatumia fedha nyingi katika utekelezaji wa miradi hiyo ili iweze kutumika kwa muda mrefu.
Aidha, Mhe. Okash amekemea vitendo vya ukatili wa kijinsia, ubakaji, unyanyasaji na vitendo vyote vinavyoenda kinyume na maadili.
Vilevile Mkuu huyo wa Wilaya ya Chemba ametoa onyo kwa Wafugaji wanaolisha mifugo yao kwenye mashamba ya Wakulima na kusema kuwa Serikali ngazi ya Wilaya imejipanga kikamilifu kuwashughulikia Wafugaji wote wataokaoenda kinyume na agizo la Serikali.
Akizungumzia kuhusu suala la Maronjoo, DC Okash amesema kuwa Serikali ngazi ya Wilaya tayari imeanza oparesheni ya kuwakamata Maronjoo hivyo amewataka Wazazi kuzungumza na na Watoto wao wenye tabia hizo kuacha mara moja.
Akihitimisha ziara yake DC Okash amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya mambo makubwa katika Wilaya ya Chemba ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kama vile miradi ya elimu. Afya, maji, umeme, barabara, ruzuku kwa Walengwa wa TASAF na mikopo ya 10% kwa Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu hivyo amewaomba Wakazi wa Kata ya Chandama na Kata ya Songolo kujitokeza kwa wingi na kupiga kura katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba, 2025.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.