- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na Shani Amanzi,
Mkuu wa wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga amewaonya watu watakaotaka kufanya udanganyifu katika zoezi hili la kitaifa la ugawaji vitambulisho kwa Wajasirimali Wadogo hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwani watakuwa wamekwenda kinyume na taratibu.
Mhe.Simon Odunga aliyazungumza hayo alipokuwa anazindua zoezi la Ugawaji wa Vitambulisho kwa Wajasirimali Wadogo wilayani Chemba Tarehe 8/1/2019 katika Ukumbi wa Godown.
“Nataka zoezi hili lisizidi siku saba na kuhakikisha mapato yanaenda vizuri bila kusahau kuhakikisha makundi ya Wajasirimali Wadogo wanapata ikiwemo wa Magenge ya chakula,Mitumba,Mafundi cherehani,Wasusi na wengineo wanaostahili katika Tarafa zote ikiwemo Mondo,Goima,Kwamtoro na Farkwa za Chemba”aliongeza kwa kusema hivyo Mhe.Odunga.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus H. Mashimba amesema katika zoezi la awali walitambua Wajasirimali 105 ambapo katika kata ya Chemba walipata Wajasirimali 35,kata ya Kidoka Wajasirimali 40,kata ya Paranga Wajasirimali 30 na zoezi hilo limehakikiwa na Kitengo cha Biashara kwa kushirikiana na ofisi ya Mkurugenzi pamoja na Maendeleo ya Jamii.
Aidha Dkt.Semistatus H.Mashimba amesema” Kamati ya zoezi la Ugawaji wa Vitambulisho kwa Wajasirimali Wadogo ilizungunga wilaya nzima katika kutoa elimu na kuhakikisha zoezi hili linakuwa endelevu na tulibaini kuna watu walitaka kufanya udanganyifu na tuliweza kutatua jambo hilo na kuhakikisha hali hiyo haitatokea tena”
Jumla ya Vitambulisho vya Wajasirimali Wadogo 2750 kutoka Ofisi ya Rais –Tamisemi viligaiwa Mkoani ambapo walikabidhi Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mhe.Odunga ambapo aliagiza Mkurugenzi Dkt.Mashimba kuratibu zoezi hilo la Ugawaji Vitambulisho kwa wilaya yake.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.