- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na Shani Amanzi,
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga afanya uzinduzi wa shughuli ya Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya na kusema zoezi la kuanza ujenzi halikuanza hivihivi bali nguvu ya Madiwani kwa Wananchi bila kusahau Mbunge wao wa jimbo la Chemba Mhe.Juma Nkamiah kwa kuhimiza kwa nguvu akiwa bungeni kwa kutaka Chemba kupata kipaumbele kwenye Vituo vya Afya hadi kwenye Hospitali ya Wilaya.
Mhe.Simon Odunga aliongeza kwa kusema ujenzi huu unatakiwa kukamilika ndani ya miezi mitatu kuanzia sasa na tunatakiwa majengo saba ambapo hakuna jengo la Upasuaji na Mochwari na wodi mbalimbli lakini wakishirikiana kwa pamoja Wanasiasa,Mkurugenzi wa Halmashauri pamoja na Wataalam wake na Wananchi wanaweza kuikamilisha Hospitali.
“Kiukweli Serikali ya Awamu ya Tano ya Mhe.Rais John Pombe Magufuli ni ya utekelezaji zaidi na tuna haki ya kumpongeza na kujidai kwani Chemba imepata fedha mara tatu kwa mpigo kwenye Vituo vya Afya ambapo Kituo cha Afya cha Hamai tumepata milioni 600/=,Kituo cha Afya Mrijo tumepata milioni 700/= na Kituo cha Afya cha Kwamtoro tumepata milioni 700/= lakini bado Serikali yetu imetupatia tena bilioni moja na nusu kwa kila wilaya ambazo hazina hospitali za wilaya, ikiwemo Chemba ’’aliongeza kwa kusema hivyo Mhe.Simon Odunga.
Mhe.Simon Odunga alifanya uzinduzi huo akiwa na Wananchi wa Chemba,Wafanyakazi wote wa Wilaya ya Chemba,Wanasiasa wa Chemba bila kusahau Baraza la Wazee katika eneo la Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya,Tarehe 11/1/2019.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.