- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na Shani Amanzi,
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga ampongeza Mhe.Rais John Pombe Magufuli kwa hatua alizochukua kwa kuruhusu baadhi ya vijiji vilivyokuwa kwenye Hifadhi ya Taifa vyenye watu wengi vibaki na kwa upande wa vijiji vingine ambavyo vimesajiliwa kimakosa wakati vipo kwenye Hifadhi Wizara tatu husika ziweze kuwajibika katika maeneo husika yaliyopo kwenye Hifadhi .
Mhe.Odunga "Ningependa kuomba ushirikiano kwa Wizara husika tatu ikiwemo Ofisi ya Rais-TAMISEMI,Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi zije ili tuweze kukaa kwa pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Chemba,Uongozi wa Pori la Akiba Swagaswaga na Serikali ya kijiji cha Handa kwa nia ya kujadili hatma ya huu muingiliano wa mipaka"
"Aidha kumekuwa na muungiliano hasa tukitaka kuleta shughuli za kimaendeleo katika jamii ambazo zipo kwenye hifadhi kwani baadhi ya Wananchi wanakataa hata kuchangia na kudai hawaelewi wapo upande gani aidha wa kubaki au kuondoka na kwa upande wangu nisengependa Swagaswaga kuwa shamba la bibi kwani baadhi ya Wananchi wanajua wanavuka mipaka lakini bado wanaendelea kuingia ndani ya pori na kuharibu mazingira kwa kukata miti ovyo na kufanya shughuli za kilimo."aliongeza kwa kusema hivyo Mhe.Odunga.
Kijiji cha Handa kilibidi kibadilishwe mpaka wa kijiji na Hifadhi ya Swagaswaga lakini kuna watu bado wapo ndani ya Hifadhi kabisa ambapo kuna vitongoji viwili vipo ndani ya Hifadhi havipo kwenye muingiliano vitongoji hivyo ni kitongoji cha Ilala"A" na Ilala ''B"
Mhe.Simon Odunga aliyazungumza hayo alipokuwa na Waandishi wa Habari ofisini kwake, Tarehe 17/1/2019 wilayani Chemba.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.