- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na Shani Amanzi,
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga ametoa agizo kwa Wananchi wa Wilaya ya Chemba katika kata ya Mrijo wanaoishi mabondeni kuhama maeneo hayo kama alivyoagiza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Binilith Mahenge alipotembelea kata hiyo tarehe 9/1/2018.
Mhe. Odunga alisema hayo alipofanya ziara ya kuangalia hali inavyoendelea katika kata ya Mrijo tarehe 10/1/2018 alipokuwa na Kamati ya Maafa ya Wilaya ya Chemba.
Wilaya ya Chemba imeanza kupata mvua za msimu kuanzia mwezi Novemba 20 katika maeneo machache na mvua hizi zimekuwa za wastani na juu ya wastani ambapo mpaka sasa ni mm 232 na hivyo kusababisha madhara kwa baadhi ya Wananchi na mali zao.
Kata ya Mrijo ni miongoni mwa maeneo yaliyopata madhara makubwa ya mvua zilizonyesha kuanzia usiku wa tarehe 8-9/1/2018 katika vijiji vya Kaloleni ,Mrijo chini na Olboloti .
Maeneo mengine yaliyopata madhara ni kata ya Chemba katika kijiji cha Chambalo ambapo nyumba 60 zilizingirwa na maji na ng’ombe 14 walizama katika kijiji cha Mondo kata ya Mondo kutokana na mvua zilizonyesha.
Miundombinu ya barabara za Chemba-Kiteto ,Chandama-Soya ,Kimaha-Soya zimeharibika na hazipitiki kabisa wakati barabara za Kwamtoro –Sanzawa ,Kwamtoro-Lahoda,Cheku-Kelema zimeharibika na hazipitiki kwa urahisi.Pia huduma ya umeme na maji safi na salama katika vijiji vya Kaloleni ,Mrijo chini na Olboloti hazipatikani.
Madhara haya yamesababisha kifo cha kijana mmoja mwenye umri wa miaka 35 aitwaye Teo Sekali wa kijiji cha Mwaikisabe kata ya Kimaha.
Kwa ujumla taarifa hii ni ya awali ikielekeza hali halisi ilivyokuwa katika eneo la tukio mpaka sasa,athari zilizojitokeza ,changamoto,hatua zilizochukuliwa ,idadi kamili ya wahanga na mahitaji yao.
KIJIJI
|
IDADI YA NYUMBA ZILIZOANGUKA KUTOKANA NA MAJI
|
IDADI YA NYUMBA ZILIZOZINGIRWA NA MAJI
|
KAYA ZILIZOATHIRIKA
|
IDADI YA WATU WALIOATHIRIKA
|
MAHITAJI YA CHAKULA KWA WAATHIRIKA KWA SIKU 30(TANI)
|
MALI ZILIZOHARIBIKA
|
OLBOLOTI
|
87
|
650
|
270
|
1698
|
-Tani 30 za nafaka,Tani 15 za mazao jamii ya mikunde, Lita 1000 ,sukari kg 530, Chumvi 6oo
|
-Mahindi gunia 25na debe3,Alzeti gunia 1 na debe3,kuku 26,Bata 7,Mbuzi 7,Ng’ombe 2 na maharage debe 3
|
KALOLENI
|
26
|
27
|
28
|
196
|
-Tani 4 za nafaka,tani 2 za mimea jamii ya mikunde,lita 100 za
Mafuta ya kupikia ,sukari kg 20,chumvi kg 50 |
-Tani 4 za Nafaka,tani 2 za mimea jamii ya mikunde,lita 100 za mafuta ya kupikia,sukari kg 20,chumvi kg 50
|
JUMLA
|
122
|
679
|
307
|
1943
|
-TANI 35 ZA MAHINDI
|
|
Hatua za awali zilizochukuliwa na timu ya Maafa ya Wilaya na kata ni kuwahamisha watu wote wenye nyumba zilizozingirwa na maji, wananchi waliokosa makazi walihifadhiwa kwa ndugu/jamaa na wengine walihifadhiwa katika madarasa ya shule ya msingi Mrijo chini. Pia mali za waathirika wa mafuriko ziliorodheshwa na kuhifadhiwa kwenye maghala ya Olboloti na Mrijo chini kwa usalama zaidi.
Vilevile, Jeshi la zima moto na uokoaji Mkoa wa Dodoma lilifanikiwa kutoa huduma ya uokoaji wa kaya 31 katika kitongoji cha Kaloleni walioshindwa kuvuka maji. Wahanga waliandikishwa majina na Wenyeviti wa Vitongoji chini ya utaratibu wa kamati ya maafa ya wilaya na masomo kwenye shule ya Sekondari Mrijo na kituo cha utayari Kaloleni yalisitishwa mpaka hapo hali itapokuwa shwari.
Changamoto walizokumbana nazo Kamati ya maafa kuanzia mwanzo wa tukio ni uhaba wa vyombo vya usafiri mfano magari, baadhi ya Wananchi kutotii maagizo toka kwa Viongozi ya kuwataka kuhama maeneo hatarishi,Wilaya kukosa vyombo vya uokoaji kwa ajili ya kutoa huduma kwa wakati na hivyo kusubiri vifaa kutoka Mkoani, kuharibika kwa miundo mbinu ya barabara na kusababisha kuchelewesha utoaji wa huduma kwa wakati.
Mhe.Simon Odunga amezitaja hatua zilizochukuliwa na Uongozi wa Wilaya ya Chemba ni kutoa “gunia 20 za Unga wa mahindi,maharage gunia 5,sukari kg 100,mafuta ya kula lita100, vifaa tiba na water guard kwa ajili ya maji ya kunywa”
Aidha Mhe.Odinga amesema pamoja na hatua za awali zilizochukuliwa na Wilaya ,Kamati ya Maafa ya Wilaya inaomba kusaidiwa kupata mahitaji yalioanishwa kama ifuatavyo tani 35 za nafaka,tani 17.25 za mazao jamii ya mikunde,lita 113 za mafuta ya kula ,sukari kg 620,tanki 4 za lita 10000 za kuhifadhia maji,katoni 700 za maji ya kunywa,magodoro 1000,blanketi 1000 na dawa za vifaa tiba.
“ Wilaya ya Chemba inaendelea kufanya tathmini ya maeneo watakayohamishwa kwa ajili ya makazi waathirika wote wa mafuriko pamoja na kuwapatia huduma muhimu kama vile vyakula na ulinzi na tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Mkuu wa Mkoa Mhe,Binilith Mahenge,Kamati yake ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Chemba Mhe.Juma Nkamia kwa kufika katika kata ya Mrijo kuwafariji waathirika wa mafuriko”alihitimisha kwa kusema hayo Mhe.Simon Odunga.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.