- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Saturday 23rd, September 2023
@Chemba District
Na Shani S. Amanzi,
Mwenyekiti wa Alat Mkoa –Dodoma Mhe.White Zuberi amefurahishwa na kasi waliyonayo Viongozi,Wafanyakazi na Wananchi katika kushiriki kwenye shughuli za kimaendeleo kwa kujionea wenyewe walipokuja Chemba.
Alat Mkoa- Dodoma iliyoshirikisha Halmashauri nane za Mkoa wa Dodoma imefanya ziara ya siku mbili kuanzia Tarehe, 25/5/2019 mpaka Tarehe ,26/5/2019 katika Wilaya ya Chemba ikiwa na lengo la kukagua miradi mbalimbali.
Ziara hiyo wametembelea miradi mitatu ikiwemo Mradi wa Bwawa la Umwagiliaji Kidoka,Shule Shikizi ya Masimba na Hospitali ya Wilaya ya Chemba ambayo ipo kwenye hatua za mwisho.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kondoa Mhe.Hamza Mafita aliuliza kuwa kuna baadhi ya Halmashauri wanapata changamoto ya manunuzi kwa upande wa Halmashauri ya Chemba wanafanyaje kwa upande wa Hospitali ya Wilaya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chemba Dkt.Semistatus H.Mashimba alijibu kwa kusema " huwa tunafatilia mara kwa mara mafundi ,onyo la barua kwa wasimamizi wa mafundi,na wakati mwingine binafsi huenda paka madukani Dodoma mjini napokuwa na vikao kufatilia vifaa vimefikia wapi. "
Aidha katika ziara hiyo walishauri kwa upande wa Mradi wa Umwagiliaji uliopo kata ya Kidoka umechukua muda mrefu unapaswa kukamilika mapema na kutafuta masoko ya mazao watakayokamilisha mapema .
Kwa upande wa Shule Shikizi ya Masimba wamepongeza kwa kuendelea vizuri na kuongeza majengo ili iweze kusajiliwa kwa sababu ni kijiji kipya cha Masimba ambapo ndipo shule ilipo.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.