- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
"Hongereni sana, katika miradi yote tuliyoipitia Siku ya Leo mmeitekeleza kwa ufanisi mkubwa, miradi yote imekamilika kwa asilimia kubwa, hii inatuonyesha kuwa Chemba kuna usimamizi mzuri wa fedha za Serikali muendelee hivyo hivyo"
Pongezi hizo zimetolewa tarehe 12, Agosti 2025 na timu ya Wataalamu wa ufuatiliaji na tathimini kutoka TAMISEMI ambao wamefika Halmashauri ya Wilaya ya Chemba kwaajili ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo, BOOST, SEQUIP na miradi iliyotekelezwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu.
"Tutawatumia kama mfano katika Halmashauri zingine ambazo zimeshindwa kutekeleza miradi kama hii, tumefurahi sana pia kuona miradi ya BOOST na SEQUIP tuliyoikagua Siku ya Leo imekamilika na mingine imeanza kutumika, tuna imani kuwa January 2026 tutaleta Wanafunzi hapa"'amesema Ndugu Robert Sabwoya ambaye ni Mchumi Mwandamizi kutoka TAMISEMI
Aidha timu hiyo ya Wataalamu kutoka TAMISEMI imesisitiza juu ya utunzaji wa miradi hiyo na kuongeza kuwa Serikali imetumia fedha nyingi katika utekekezaji wa miradi hiyo, hivyo ni vyema itunzwe ili iweze kutumika kwa muda mrefu.
Miradi iliyokaguliwa na timu hiyo ni Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Chemba (Chemba Boys) Shule ya Sekondari Kidoka, Nyumba za Watumishi, Nyumba ya Mkurugenzi, pamoja na Jengo la Utawala La Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.