- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na Shani Amanzi,
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe. Simon Odunga achukizwa na Wananchi na Wafanyakazi wa Serikali wasiokuwa wawajibikaji hasa pale wanapopewa majukumu na Serikali ikiwemo kuwekwa kwenye Kamati za shughuli za kimaendeleo katika jamii.
Mhe.Simon Odunga aliyazungumza hayo alipotembelea kata ya mrijo akiongozana na mkurugenzi wa Halmashauri, Katibu Tawala pamoja na wataalam wa Halmashauri walipokuwa wanaangalia hatua zilipo fikia katika utekelezaji wa kuanza kujenga Kituo cha Afya cha Mrijo, Tarehe 12/1/2019.
Mhe.Odunga amesema “nampongeza Rais wa Awamu ya Tano Mhe.John Pombe Magufuli kwa kuweka kipaumbele katika Afya na kutaka kila kata kuwena Kituo cha Afya na sitakubali mwananchi au mtaalam yoyote akwamishe malengo hayo kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa”
Aidha Mhe.Odunga aliongeza kwa kusema mkumbuke wapo Wananchi ambao baadhi yao wapo macho na wanataka kushirikishwa katika kila jambo na inasikitisha sana Kamati hii yaUjenzi inafanya mambo bila kuwashirikisha Wananchi na ninaamuru Kamati hii ivunjwe nakutaka Mkurugenzi ahakikishe ana unda nyingine mara moja kuanzia leo kwani wengi wao wananchi hawaiamini Kamati hii ikiwemo na upande wa manunuzi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chemba Dkt.Semistatus.H.Mashimba ameomba ushirikiano kwa Wananchi katika kuhakikisha Ujenzi wa Kituo cha Afya- Mrijo kinakamilika na kuipongeza Serikali katika kuweka kipaumbele katika Ujenzi waVituo vyaAfya.
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.