- Mwanzo
- Kuhusu Sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
MAAGIZO YA MKUU WA WILAYA
WAKATI WA ZIARA YAKE KWENYE VIJIJI VYA MAKORONGO NA MAZIWA
TAREHE 18&19/Novemba/2017
S/N |
AGIZO |
WAHUSIKA |
1 |
Wavamizi wa Msitu wa Hifadhi wa Kijiji cha Makorongo waondoke ndani ya siku 14 kuanzia tarehe 18/11/2017 |
-Afisa Misitu -Afisa Mazingira -Serikali ya Kijiji |
2 |
Mgogoro wa mipaka kati ya vijiji vya Makorongo na Chase utafutiwe ufumbuzi haraka |
-Afisa Ardhi -Serikali ya Kijiji |
3 |
Motor ya PUMP ya maji ilioharibika itengenezwe haraka ndani ya wiki moja kuanzia tarehe 18/11/2017 |
-Mhandisi wa Maji -Serikali ya Kijiji |
4 |
Wajumbe wa Kamati ya Maji waliohujumu fedha za mfuko wa maji wawajibishwe haraka |
-Mkaguzi wa Ndani wa H/W -Mhandisi wa Maji |
5 |
Mchakato wa kumpata Mwenyekiti mpya wa Kijiji pamoja na baadhi wa wenyeviti wa vitongoji ufanyike haraka |
-Afisa Utumishi -Afisa Uchaguzi |
6 |
Hatua kali za kisheria zichukuliwe kwa watu wote wanaoharibu Mazingira katika Kijiji cha Maziwa |
-Afisa Misitu -Afisa Mazingira -Serikali ya Kijiji |
7 |
Mpaka ifikapo tarehe 26/11/2017, kaya zote katika Kijiji cha Maziwa ziwe na vyoo |
-Afisa Mtendaji wa Kijiji -Afisa Afya |
8 |
Kaya zote ziwe kwenye mpango wa bima afya ya jamii (CHF) |
-Afisa Mtendaji wa Kijiji -Mratibu wa CHF |
9 |
Taasisi zote za umma ziwe na bendera ya Taifa |
-Afisa Utumishi |
10 |
Zao la ufuta lipewe kipaumbele ili kukabiliana na ukame |
-Afisa Kilimo |
Chemba District Council
Sanduku la Posta: 830 CHEMBA
Simu ya Mezani: 0262360175
Simu ya Mkononi: 0765980765
Barua pepe: ded@chembadc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chemba . Haki zote zimehifadhiwa.